Swalah ya ambaye amesujudu sijda moja badala ya mbili

Swali: Imamu ameswali swalah ya ´Aswr na katika Rak´ah ya mwisho akasujudu sijda moja peke yake na akaketi Tashahhud ya mwisho na akatoa Tasliym. Baada ya hapo akazinduliwa na baadhi ya waswaliji kwamba amesujudu sijda moja peke yake na hakusujudu sijda ya pili katika ile Rak´ah ya mwisho. Kisha akasimama na akawaswalisha Rak´ah nyingine kamilifu ambapo akaketi katika Tashahhud kisha akatoa Tasliym na kusujudu sijda ya kusahau. Je, sifa hii ni sahihi?

Jibu: Ndio, haya ndio yamewekwa katika Shari´ah. Imamu akisahau sijda ambapo akatoa Tasliym halafu akakumbuka au akazinduliwa, basi atasimama na kuswali Rak´ah nyingine, kisha atakamilisha, kisha atatoa Tasliym halafu atasujudu sijda ya kusahau baada ya Tasliym, jambo ambalo ndio bora zaidi. Vivyo hivyo anayeswali peke yake ana hukumu moja kama yeye. Akisujudu sijda ya kusahau kabla ya Tasliym ni sawa pia. Lakini bora afanye hivo baada yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/277)
  • Imechapishwa: 01/11/2021