Ametaka kuzidisha masiku juu ya masiku aliyojiwekea kufanya I´tikaaf

Swali: Kuna mtu amenuia kufanya I´tikaaf siku saba kisha baada ya hapo akanuia kuendelea. Je, akate I´tikaaf yake na aanze I´tikaaf kwa nia mpya? Kwa msemo mwingine ni kwamba abaki katika ile nia yake ya kwanza?

Jibu: Akinuia kufanya I´tikaaf siku saba basi anatakiwa kufanya I´tikaaf siku saba kisha aikate I´tikaaf yake. Kwani anatakiwa kupambanua I´tikaaf ya wajibu na isiyokuwa ya wajibu. Kwa hivyo anapaswa kutoka nje ya I´tikaaf baada ya siku saba. Baada ya hapo hakuna neno akitaka kufanya I´tikaaf. Katika jambo hili kuna kujichokesha. Mtu anatakiwa asiichokeshe nafsi yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika dini hii ni nyepesi.”

Midhali ameweka nadhiri ya kufanya I´tikaaf siku saba basi analazimika kutoka baadaye na astarehe. Baada ya kustarehe akitaka kufanya I´tikaaf iliyopendekezwa, basi hakuna neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 01/03/2019