Ameswali ndani ya ndege kwa kukaa ilihali anaweza kusimama


Swali: Niliswali ndani ya ndege kwa kukaa chini pamoja na kujua kwamba naweza kusimama na nafasi ipo. Je, niirudi swalah yangu?

Jibu: Ndio. Ni lazima kwako kuirudi swalah yako ikiwa ulikuwa unaweza kusimama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Imraan bin Huswyan:

“Swali kwa kusimama, ikiwa huwezi kwa kukaa chini, ikiwa huwezi kwa ubavu.”

Akiswali kwa kukaa chini ilihali anaweza kusimama basi swalah yake si sahihi ikiwa ni swalah ya faradhi. Ama ikiwa ni swalah ya Naafilah hakuna neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 08/05/2019