Kila ambavyo swawm inambamba mtu ndivo thawabu zinakuwa nyingi

Swali 407: Mfungaji akitumia sehemu kubwa ya mchana wake akipumzika kwa sababu ya njaa na kiu kali – je, kitendo hicho kinaathiri juu ya kusihi kwa swawm yake?

Jibu: Hili haliathiri kusihi kwa swamw yake. Ndani yake kuna thawabu zaidi kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Aaishah:

“Ujira wako ni kwa kiwango cha kuchoka kwako.”

Kila ambavyo mtu kuchoka zaidi katika kumtii Allaah basi ndivo thawabu zake zinavyozidi. Inafaa kwake kuyafanya yale mambo ambayo yatampunguzia swawm yake kama kujimwagia maji kwa ajili ya kupata baridi kidogo na kukaa sehemu ya kijibaridi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 466
  • Imechapishwa: 08/05/2019