Amesahau kuosha uso katika wudhuu´

Swali: Kuna mtu amesahau kuosha uso wake wakati wa kutawadha kisha alipomaliza viungo vyote akaosha uso wake. Je, inatosha kufanya hivo au ni lazima kurudi kutawadha upya?

Jibu: Arudi kile alichosahau na vile viungo vilivyofuatia baada yake kwa sharti viungo vyake visivyo vimeshakauka. Ikiwa vimeshakauka basi ni lazima kutawadha upya tena.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (104) https://www.alfawzan. af.org.sa/sites/default/files/13-03-1441%D9%87%D9%80~1_0.mp3
  • Imechapishwa: 03/01/2021