Amesahau ´ishaa mpaka wakati wa Fajr

Swali: Nimesahau kuswali ´Ishaa na nimekuja kuikumbuka saa moja kabla ya swalah ya Fajr. Katika hali hii niiswali?

Jibu: Ndio. Wakati wa ´ishaa unabaki mpaka kupambazuke alfajiri. Mwenye kuwahi Rak´ah moja katika swalah ya ´ishaa kabla ya kuingia Fajr ameiwahi swalah ya ´ishaa. Aharakishe kuiswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (71) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-06-13.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020