Swali: Kuna mtu kanuwia safari asubuhi na akanuwia kula lakini hakusafiri. Atimize swawm yake au ale na alipe siku ile?

Jibu: Akiadhini muadhini adhaana ya pili naye bado yuko na nia hii ya safari na ya kula, kisha baada ya hapo hakusafiri atakata swawm yake na atalipa siku nyingine kwa kuwa nia yake imekatika. Au kwa kuwa alinuwia kula, atalipa siku nyingine. Na ikiwa alikula baada ya Fajr pia atakata swawm yake na kulipa siku nyingine. Na ikiwa hakula wala kunywa atakata swawm yake na kulipa siku nyingine. Na ikiwa aliwahi kuweka nia kabla ya adhaana ya Fajr ya kufunga, akafunga hana juu yake kitu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020