Allaah analipa kwa kitendo na si kwa ujuzi

Swali: Kuna utata umenitatiza, nao ni kwamba, Allaah (´Azza wa Jalla) Anajua kwa Ujuzi Wake uliotangulia ya kwamba Ibraahiym (´alayhis-Salaam) atatekeleza maamrisho kwa kuchinja. Kwa nini basi Allaah (´Azza wa Jalla) Amwamrishe kufanya hivo ilihali anajua hilo?

Jibu: Ndugu! Haya ni masuala ya ajabu. Allaah Haadhibu kwa Ujuzi au Akatoa ujira kwa Ujuzi. Anatoa ujira kwa sababu ya kitendo. Anajua kuwa kafiri atakua kafiri, lakini hamuadhibu mpaka pale ambapo kafiri atapotenda. Anajua kuwa Muislamu atakuwa Muislamu, lakini hampi thawabu mpaka pale ambapo yeye mwenyewe atapotenda. Malipo yanatokana na matendo na hayatokani na Ujuzi wa Allaah tu. Tambueni hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-5-11.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014