Swali: Kuna mtu mwanzoni mwa kubaleghe kwake alikuwa akifunga swawm sahihi lakini hata hivyo alikuwa anajichua sehemu ya siri. Alikuwa ni mjinga na hajui kabisa kwamba jambo hili linaharibu swawm na kwamba linawajibisha kuoga. Alikuwa anaswali na anafunga na wakati huohuo anajichua. Haya yalikuwa mwanzoni mwa kubaleghe kwake ambapo alikuwa chini ya miaka kumi na tano. Kipi kinachomlazimu baada ya kujua hukumu na akatubu kwa Allaah? Hajui ni masiku mangapi alijichua na vilevile swalah.

Jibu: Kuna makosa katika swali hili. Anasema kabla ya kubaleghe ilihali anatokwa na manii. Je, ibara hii ni sahihi? Hapana. Kwa sababu akitokwa na manii kwa ladha ina maana kwamba amekwishabaleghe japokuwa atakuwa na miaka kumi tu. Lakini tunamjibu kwa kusema, midhali anafanya hivo kipindi cha funga na wakati huohuo alikuwa hajui kuwa ni haramu, basi swawm yake ni sahihi. Tulitaja kanuni hii.

Kuhusu upande wa swalah ambapo alikuwa anaswali pasi na kuoga na wakati huohuo alikuwa hajui kuwa kitendo hicho kinamuwajibishia mtu kuoga, vivyo hivyo sio lazima kulipa. Kwa sababu alikuwa mjinga. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuwajibishia mtu yule ambaye alikuwa anaacha nguzo katika swalah. Namaanisha yule mtu ambaye aliingia msikitini na akaswali swalah ya kudonoa. Baada ya hapo akaja na kumtolea salamu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Rudi uswali! Kwani hakika hujaswali.” Akarudi na akaswali kama mara ya kwanza na akarudi, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamrudisha mara tatu. Hakumwamrisha kuzilipa swalah zake zilizotangulia pamoja na kuwa alimwambia: “Kwani hakika hujaswali.” Hivyo namwambia muulizaji huyu kwamba haimlazimu kulipa swalah zako wala kulipa swawm zako. Lakini nakuuasia kufanya matendo mema kwa wingi na kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1176
  • Imechapishwa: 06/07/2019