Tunajua maana ya sifa za Allaah na hatujui namna

Swali: Baadhi ya watunzi wa vitabu walioko masokoni na kwenye maduka wanathibitisha kwamba madhehebu ya Salaf ni kumtegemezea Allaah maana na namna.

Jibu: Hapana, si sahihi. Walikuwa wakitegemeza namna pekee. Wanaosema kwamba walikuwa wakitegemeza maana ni kosa. Madhehebu ya Salaf ni kutegemeza namna pekee. Tunajua maana ya Mwingi wa huruma, maana ya Mwenye kurehemu, maana ya Mwenye kusikia kila kila kitu, Mwenye kuona kila kitu, maana ya Mwenye nguvu asiyeshindika na Mwingi wa hekima. Lakini hatujui namna zake. Hatujui namna Allaah alivyolingana na namna ya elimu Yake. Hatujui namna.

Swali: Kuegemeza maana ni madhehebu ya Mufawwidhah?

Jibu: Ndio, ni madhehebu ya Mufawwidhah. Ni madhehebu batili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 83
  • Imechapishwa: 06/07/2019