Swali: Katika gazeti la “al-Mujtamaa´”[1] al-Qardhwaawiy anasema kuwa inajuzu kwa mwanamke kuwa mwigiza [mchezaji filamu]:

“Dalili yangu ni vile visa vya Qur-aan tangu wakati wa Aadam (´alayhis-Salaam) mpaka wakati wa Mtume wa mwisho (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kote mwanamke ameshiriki; Aadam na Hawwaa´, Nuuh na mkewe, Luutw na mkewe, Ibraahiym na mkewe, kisa cha watoto wawili wa kiume wa Aadam, kisa cha Muusa tangu kuzaliwa kwake ilipozungumzia mama yake na dada yake na mke wa Fir´awn na wasichana wa Shu´ayb na mijadala yao na Mtume wa Allaah Muusa, Yuusuf na mke wa mfalme, Suurah nzima iliyozungumzia kuhusu mwanamke aliyecheza kazi yenye nafasi ya juu, ´Iysaa na mama yake na maelezo ya mama yake yamepambanuliwa na Zayd bin al-Haarithah na mke wake Zaynab bint Jahsh. Qur-aan imetaja visa vyote hivi ambapo ndani yake mwanamke anacheza nafasi ya juu kabisa. Ni vipi basi tutamfungia mlango mbele yake na kumtoa katika maisha yake?

Halafu akataja vidhibiti vya yeye kujiingia katika maigizo.

Jibu: Mtu huyu lau atakuwepo mtu wa kumkufurisha sintomkosoa. Lakini hata hivyo mimi nasema kuwa ni mpotevu aliyepotea upotevu wa wazi. Kwa nini? Kwa kuwa anamnasibishia Allaah na Qur-aan uongo. Mimi nikiigiza na kusema kuwa ni Abu Bakr na mwengine ni Abu Jahl, je hivi kweli mimi ni Abu Bakr na huyo mwengine ni Abu Jahl? Hapana. Ina maana kuwa tunamnasibishia Allaah na Qur-aan uongo. Maigizo ni uongo na dogo linaloweza kusemwa ni kwamba ni uongo.

[1] Nambari 1319. 1419/06

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 74
  • Imechapishwa: 08/10/2016