Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa al-Haakimiyyah ni miongoni mwa ´ibaadah maalum kabisa?

Jibu: Hapana. al-Haakimiyyah ni tawi la hukumu ambazo ni lazima kwa mtawala kuhukumu kwazo. Ni lazima kwa mtawala kuhukumu kwa Shari´ah. Akihukumu kinyume na Shari´ah kwa kukusudia hali ya kuwa ni mwenye kuhalalisha kitendo hicho anakufuru. Lakini akihukumu kwa matamanio na kwa sababu ya rushwa anakuwa ni mtenda maasi na maovu ni kufuru ndogo. Ni miongoni mwa masuala ya Shari´ah yenye kufuata Tawhiyd-ul-´Ibaadah.

Swali: Je, masuala ya al-Haakimiyyah na kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah yanaingia katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah au Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah?

Jibu: Inategemea. Wakati fulani yanaingia katika ukafiri. Wakati mwingine yanaingia katika maasi na kufuru ndogo kama mfano wa uzinzi na unywaji pombe. Akiona kuwa mambo hayo ni halali anakuwa kafiri. Asipoyahalalisha anakuwa ni mtenda maasi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 74
  • Imechapishwa: 23/07/2019