al-Fawzaan kuhusu nadharia ya Darwin

Swali: Kuna daktari amesema Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا

“Hali ya kuwa Amekuumbeni hatua baada ya hatua?” (71:14)

ya kwamba ndani yake kuna dalili ya nadharia ya Darwin…

Jibu: Tunajilinda kwa Allaah. Tunajilinda kwa Allaah. Darwin huyu kafiri anayesema kuwa msingi wa mwanadamu anatokamana na tumbili?

وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا

“Hali ya kuwa Amekuumbeni hatua baada ya hatua?”

maana yake ni:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن سُلَالَةٍ مِّن طِينٍ ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَةً فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا ثُمَّ أَنشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ ۚ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِين

“Kwa hakika Tumemuumba mtu kutokana na mchujo safi wa udongo, kisha tukamjaalia kuwa tone la manii katika kalio makini, kisha tukaumba tone la manii pande la damu linaloning’inia, tukaumba pande la damu hilo linaloning’inia kinofu cha nyama, tukaumba kinofu cha nyama hiyo mifupa, tukavisha mifupa hiyo nyama, kisha tukamuanzisha kiumbe kingine. Basi ametukuka Allaah, Mbora wa wenye kuumba.” (23:12-14)

kama ilivyokuja katika Suurat-ul-Mu´minuun.

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن سُلَالَةٍ مِّن طِينٍ ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَةً فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا

“Kwa hakika Tumemuumba mtu kutokana na mchujo safi wa udongo, kisha tukamjaalia kuwa tone la manii katika kalio makini, kisha tukaumba tone la manii pande la damu linaloning’inia, tukaumba pande la damu hilo linaloning’inia kinofu cha nyama… “

hii ndio hatua baada ya hatua. Au hatua kwa hatua ni pale baada ya kutoka kwenye tumbo la mama yake, anaenda katika daraja ya utoto, kisha daraja ya kuweza kupambanua, kisha daraja ya kubaleghe mpaka mwisho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-10.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020