Swali: Msichana mdogo ambaye amevaa Hijaab na ambaye ameshikamana na vazi la Kiislamu lililowekwa katika Shari´ah na anausitiri mwili wake mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono. Je, anaruhusiwa akitaka kuswali kila nyakati ya swalah msikitini kufanya hivo? Je, anaruhusiwa daima kwenda na mume wake?

Jibu: Hapana vibaya kwa mwanamke kuswali msikitini akiwa ni mwenye kujisitiri Hijaab inayokubalika katika Shari´ah na hali ya kuwa amefunika uso wake, viganja vyake vya mikono na mwili wake mzima. Sambamba na hayo ajiepushe na manukato na kuonyesha mapambo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah na misikiti ya Allaah.”

Lakini bora ni yeye kuswali nyumbani kwake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… na nyumba zao ni bora kwao.”[1]

[1] Ahmad (5211) na Abu Daawuud (480).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/80)
  • Imechapishwa: 20/11/2021