Swali: Je, akatazwe ambaye anafunga mwezi wote wa Muharram na ambaye anafunga Sha´baan na akaifuatishia na Ramadhaan?

Jibu: Asikemewe. Kuhusu Muharram Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swawm bora baada ya mwezi Ramadhaan ni mwezi mtukufu wa Allaah Muharram.”

Kuhusu funga ya Sha´baan imethibiti katika “as-Swahiyh”:

“Ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga Sha´baan yote.”

“Alikuwa anafunga [masiku mengi ya] Sha´baan isipokuwa [masiku] machache.”

Akifunga yote au akala masiku yake machache ni vizuri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 15/10/2021