Aina mbalimbali za maimamu na hukumu ya kuswali nyuma yao

Aina za maimamu:

1- Imamu ambaye hali yake imejificha. Huyu ni yule imamu ambaye hajulikani kuwa na Bid´ah na maovu. Kuswali nyuma ya imamu huyu inajuzu kwa makubaliano ya maimamu wote. Sio miongoni mwa masharti ya uimamu maamuma wajue yale ambayo imamu anaamini na kumpa mtihani kwa kumuuliza nini anachoitakidi.

2- Kuswali nyuma ya mtu wa Bid´ah ambaye analingania katika Bid´ah zake na mtenda dhambi ambaye anadhihirisha maasi yake. Kuna wanachuoni waliofafanua na kusema ikiwa analingania katika Bid´ah zake hakuswaliwi nyuma yake. Na ikiwa halinganii katika Bid´ah zake kunaswaliwa nyuma yake. Vilevile inahusiana na mtenda dhambi. Ikiwa anadhihirisha maasi yake hakuswaliwi nyuma yake. Na ikiwa hadhihirishi maasi yake kunaswaliwa nyuma yake. Usawa ni kwamba ni sahihi kuswali nyuma yake kwa sharti isiwe Bid´ah zake zinamfikisha katika kiwango cha kufuru. Kadhalika isiwe ufuska wake unamfikisha katika kiwango cha kufuru.

3- Imamu kafiri. Haisihi kuswali nyuma yake kwa makubaliano. Kwa mfano mwenye kuabudu makaburi ambaye anaomba asiyekuwa Allaah, anachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, anatufu kwenye makaburi au anawawekea nadhiri maiti, hakuswaliwi nyuma yake. Kukiswaliwa nyuma yake basi mtu arudi swalah yake, sawa ikiwa utajua hali yake wakati uko unaswali, kabla ya kuanza au baada ya swalah. Inatakiwa kurudi kuswali swalah yako hata kama itakuwa baada ya muda mrefu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/534-535)
  • Imechapishwa: 19/05/2020