Adhaana ya kwanza katika swalah ya Fajr imependekezwa

Swali: Je, imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alihimiza adhaana ya kwanza kwa ajili ya Fajr? Kuna muda kiasi gani kati ya adhaana ya kwanza na adhaana ya pili?

Jibu: Adhaana ya kwanza imependekezwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bilaal anaadhini usiku. Hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum.”

Mpokezi amesema:

“Alikuwa ni mtu kipofu na haadhini mpaka aambiwe “kumepambazuka, kumepambazuka.”

Hii inafahamisha kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkubalia Bilaal kitendo chake na (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akabainisha hekima ya hilo kwa kusema katika moja ya mapokezi:

“Bilaal anaadhini usiku ili kumuamsha aliyelala katika nyinyi na kumrejesha aliye macho katika nyinyi… “

Katika kufanya hivo hakuna kikomo maalum. Bora adhaana ya kwanza iwe karibu na adhaana ya mwisho. Hayo ni kutokana na maneno ya mpokezi katika baadhi ya mapokezi:

“Hakukuwa kati yazo isipokuwa kitambo cha kupanda huyu na kushuka mwengine.”

Kwa msemo mwingine ni kwamba hakukuwa kazi yazo isipokuwa kitambo kifupi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/341)
  • Imechapishwa: 19/09/2021