Aache kuoga josho la hedhi na janaba kwa sababu ya nywele kupukuchika wakati wa kuziosha?

Swali: Kuna mwanamke amepatwa na maradhi yanayofanya nywele zake kupukuchipa wakati anapoziosha na maji. Afanye nini? Je, aache kuoga josho la hedhi na janaba?

Jibu: Hapana, ni lazima aoge kwa ajili ya hedhi na janaba. Nywele kupukuchika kwa kuzitia maji ni ugonjwa na maradhi. Itambulike kuwa Allaah hakuteremsha ugonjwa wowote isipokuwa pia ameteremsha dawa yake. Hivyo basi aende kwa madaktari huenda wakampatishia dawa itayozifanya nywele kuwa imara pindi atapozipitishia juu yake maji. Nakhofia mwanamke huyu akawa na wasiwasi fulani na kwamba anaosha kichwa chake kwa kukisugua sana na matokeo yake ndio maana nywele zinapukuchika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1455
  • Imechapishwa: 07/01/2020