Faida ya sita: ´Allaamah Swiddiyq Hasan Khaan amesema baada ya kutaja Hadiyth nyingi juu ya fadhilah ya kumsifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kukithirisha kufanya hivo:

“Hapana shaka yoyote kwamba waislamu wanaomsifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa wingi ni Ahl-ul-Hadiyth na wapokezi wa Sunnah safi. Hakika miongoni mwa kazi zao katika elimu hii tukufu ni kumsifu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kila Hadiyth. Ndimi zao ni zenye kuendelea wakati wote kuwa kavukavu kwa kumtaja yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna kitabu chochote cha Sunnah au cha Hadiyth isipokuwa kina maelfu ya Hadiyth. Ukiongezea juu yake tungo zengine zote za kinabii. Kundi hili lililookoka na la Hadiyth ndilo lenye haki zaidi ya kuwa karibu na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wenye furaha zaidi juu ya uombezi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Qiyaamah. Hakuna mtu yeyote anayelingana nao katika fadhilah hii isipokuwa kama mtu huyo atafanya vyema zaidi kuliko wao. Sio jambo linalofikiwa kirahisi.”

Mimi namuomba Allaah anifanye kuwa miongoni mwa Muhaddithuun hao ambao ndio watu wenye haki zaidi ya kuwa karibu na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huenda kitabu hiki ni miongoni mwa dalili ya hilo. Allaah amrehemu imaam wa Ahl-us-Sunnah, Imaam Ahmad aliyesema:

Dini ya Muhammad ni ya maelezo

njia bora kwa kijana ni ya mapokezi!

Usizipe mgongo Hadiyth na watu wake

kwa sababu maoni ni usiku na Hadiyth ndio mchana

Huenda kijana asiitambue njia ya uongofu

lakini jua liko juu waziwazi na likiangaza kwa miale yake

Kadhalika amesunisha pia kuomba du´aa katika Tashahhud hii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mnapokaa kila baada ya Rak´ah mbili basi semeni… “

Akataja Tashahhud yote mpaka mwisho kisha akasema:

“Kisha aombe kile anachokipenda.”[1]

[1] an-Nasaa’iy, Ahmad na at-Twabaraaniy kupitia kwa Ibn Mas´uud. Imetajwa katika ”as-Swahiyhah” (878) pamoja na uelewa wake. Ina mapokezi yenye kuitia nguvu katika ”Majma´-uz-Zawaa-id” (2/142) kupitia kwa Ibn-uz-Zubayr.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 153-154
  • Imechapishwa: 07/01/2019