Faida ya pili: Muheshimiwa msomaji ameona matamshi mbalimbali yote ndani yake kuna kuwasifu jamaa zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakeze na kizazi chake pamoja naye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa ajili hiyo sio Sunnah wala kuafikiana na maamrisho yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mtu peke yake kusema:

اللهم صل على محمد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad.”

Ni lazima kwa mtu kusoma sentesi/jumla yote kamilifu kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika suala hili hakuna kutofautisha kati ya Tashahhud ya kwanza na Tashahhud ya pili. Haya yamesemwa na Imaam ash-Shaafi´iy:

“Tamko katika ile Tashahhud ya kwanza na Tashahhud ya pili ni moja. Hakuna tofauti. Tashahhud maana yake ni kushuhudia na kumsifu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haisihi moja pasi na nyingine.”[1]

Kuhusu Hadiyth inayosema:

“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya Rak´ah mbili hasomi zaidi ya kushuhudia.”

Ni dhaifu sana, kama nilivyothibitisha katika “adh-Dhwa´iyfah”[2].

[1] al-Umm (1/102).

[2] 5816.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 147-148
  • Imechapishwa: 03/01/2019