4 – Miongoni mwa sababu za kuhifadhi tupu ni kukataza faragha kati ya mwanamke na mwanaume ambaye sio Mahram yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho basi asikae faragha na mwanamke ambaye hana Mahram yake  – kwani watatu wao ni shaytwaan.”

´Aamir bin Rabiy´ah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamume asikae faragha na mwanamke ambaye si halali kwake. Kwani hakika watatu wao ni shaytwaan; isipokuwa Mahram.”

al-Majid amesema katika “al-Muntaqaa´”:

“Ameipoikea Ahmad na imekwishatangulia maana yake kwa Ibn ´Abbaas katika Hadiyth iliopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim.”

Imaam ash-Shawkaaniy amesema katika “Nayl-ul-Awtwaar”:

“Kuna maafikiano juu ya kwamba ni haramu kukaa faragha na ambaye ni ajinabi, hayo yamesimuliwa na Haafidhw katika “al-Fath”. Sababu ya uharamu ni ile iliyotajwa katika Hadiyth kwamba watatu wao ni shaytwaan. Uwepo wake utawafanya kutumbukia katika madhambi. Ama kwa pamoja na kuwepo kwa Mahram kukaa faragha na ambaye ni ajinabi inafaa na kutowezekana kutokea madhambi pamoja na uwepo wake.”[1]

[1] (06/120).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 124
  • Imechapishwa: 11/12/2019