al-Halabiy hakutosheka na hilo. Tahamaki Salafiyyuun wakagundua jinsi wanavyoshambuliwa na jinsi misingi ya Salafiyyah inavyoshambuliwa kwenye vitabu vyake vingi na makala kwenye tovuti potevu ambayo ameunda kwa kila Khalafiy anayepiga vita mfumo wa Salaf na watu wake. Mashambulizi haya ya dhuluma ameyafanya kwa miaka mingi na kwa misingi haribifu ya ´Ar´uur na al-Ma´ribiy na ukiongezea mengi juu ya hayo. Isitoshe ameongeza misingi mingine dhidi ya mfumo wa Salaf.

Kwa mfano hakubali Tabdiy´ yoyote ikiwa Ummah mzima haukukubaliana nayo.

Anatilia shaka mapokezi ya waaminifu na kuonelea ya kwamba hata mapokezi ya Maswhabah ni lazima yathibitishwe [kwanza].

Ameunda msingi “Sijakinaika” hata kama kutakuja mtu wa haki kwa dalili na hoja.

Wakati mwingine anasema “Hainilazimu” ili kutupilia mbali haki ilio wazi kabisa.

Misingi yote hii ameiunda ili kupiga vita mfumo wa Salaf katika kujeruhi na kusifu, Jarh wa Ta´diyl, ushahidi wa haki na uadilifu.

Katika kipindi hichi Allaah Alimfedhehesha pindi ambapo miaka mingi alishuhudilia uongo juu ya gazeti lenye kujulikana kuwa na upotofu mkubwa kama umoja wa dini, udugu wa dini, usawa wa dini, kuwapenda watu wa dini zingine na wito wa demokrasia na kuhukumu kwa hukumu za FN. Alisifu gazeti hili na kushuhudilia batili juu ya kwamba linafafanua Uislamu na kuweka wazi upekee wake. Ukiongezea juu ya hayo ni kuwa alieleza Raafidhwah, Khawaarij, Suufiyyah na wanasekula ambao wao pia walisifu gazeti hilo kwa njia ya kwamba ni wanachuoni wenye kuaminika na viongozi waaminifu. Namna hivi ndivyo alivyoshuhudilia wakati alipojitetea na gazeti hili.

Ni mara ngapi kundi lake walilitetea! Baadhi yao walifikia kiasi cha kwamba walilifafanua kwenye mikanda khamsini ambapo ndani yake aliugeuza Uislamu. Yote haya na ukiongezea juu ya hayo mengine mengi yanapatikana kwenye tovuti “Kull-ul-Khalafiyyiyn” ambayo kwa dhuluma kubwa inajiita “Kull-us-Salafiyyiyn”.

Je, ushuhudiaji huu wa dhambi hauendi kinyume na mfumo wa Salaf ambao anadai, lakini ambao unavunja vibaya sana madai yake na kadhalika unavunja Uislamu? Pamoja na hivo anasema kuwa anamkufurisha mwenye kuamini kuwepo umoja wa dini. Ni vipi anaweza kushuhudia umoja wa dini na udugu wa dini pamoja na kundi lake wakatetea yote hayo kisha eti baadae anamkufurisha mwenye kuamini kuwepo umoja wa dini? Mpaka katika hali yake ya uandishi leo hii ameshikamana na ushuhudiaji wake wa uongo. Ni vipi vitu viwili vilivyo kinyume kabisa vinaweza kuwa kitu kimoja kwa Allaah, Waislamu na watu wenye akili timamu?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017