64. Huku ndio kupingana na Allaah kuliko kukubwa kabisa

Na yule anayemuamini mtu mwema au kitu kisichoasi, kama mfano wa mti na jiwe, ni uovu kidogo kuliko yule anayemuamini yule anayeshuhudia anafanya madhambi na ufisadi na akathibitisha hilo.

MAELEZO

Na yule anayemuamini… – Hii ndio faida ya kulinganisha kati ya shirki ya watu wa mwanzo na shirki ya waliokuja nyuma ambao wanajinasibisha na Uislamu. Tofauti yenyewe ni kwamba kushirikisha kwa kuwaabudu watu wema na viumbe visivyoasi ni jambo khafifu kuliko kushirikisha kwa kuwaabudu watenda dhambi, wakanamungu na watenda maasi. Kwa kuwa kufanya hivo kunafahamisha kuwatakasa na kuafikiana nao juu ya ukafiri wao, dhambi zao na kuyazingatia kuwa ni wema na karama – kuna kupingana na Allaah kupi kuliko kukubwa kama kufanya hivi? Tunamuomba Allaah afya!

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 95
  • Imechapishwa: 01/02/2017