60. Mwanamke amekatazwa kusindikiza jeneza makaburini


Swali 60: Ni ipi maana ya Hadiyth ya Umm ´Atwiyyah:

“Tumekatazwa kufuata jeneza?”[1]

Jibu: Malengo ya makatazo ni kukatazwa kulisindikiza makaburini. Ama kumswalia ni jambo limesuniwa kwa wanamme na wanawake. Wanawake walikuwa wakiswalia jeneza pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/178).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 45
  • Imechapishwa: 26/12/2021