51. Allaah alijidhihirisha kwenye mlima


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Alijionyesha mlimani ambapo ukapasukapasuka kutokana na utukufu Wake.

MAELEZO

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا

“Basi Mola wako alipojidhihirisha katika mlima akalifanya livurugike kuwa vumbi.”

Wakati Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposikia maneno ya Mola wake, ndipo akatamani pia kumuona na akasema:

رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ

“Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.”[1]

Allaah akamjibu:

لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي

“(Lan) Hutoniona! Lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.”[2]

Huna uwezo wa kuniona. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akataka kumbainishia hilo kwa kumuonyesha ni kipi kitachoutokea mlima ikiwa atajionyesha:

وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي

”… lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.”[3]

Mlima ulipasukapasuka na kuwa changarawe.

وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا

“… na Muusa akaanguka hali ya kuzimia.”[4]

Kwa sababu ya woga.

[1] 7:143

[2] 7:143

[3] 7:143

[4] 7:143

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 02/08/2021