Swali: Nawaona baadhi ya watu wanapoona mti umeota juu ya kaburi wanamsifu yule mtu mwenye kaburi lile kuwa alikuwa na sifa kiwango chake ni kadhaa na kadhaa. Je, kule kuota miti juu ya makaburi kuna mafungamano yoyote?

Jibu: Hakuna msingi wa jambo hilo. Kuota kwa mti na magugu juu ya makaburi ni alama ya wema ya wenye nayo. Hiyo ni dhana potofu. Miti inaota kwenye makaburi ya wema na waovu na si jambo maalum kwa watu wema. Kwa hiyo haitakikani kudanganyika na maneno ya wenye kudai kinyume na hivo katika waliopinda na watu wenye imani potofu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 140
  • Imechapishwa: 26/07/2022