Nia ya Istikhaarah mwishoni mwa swalah ya Raatibah

Swali: Nikiswali sunnah ya Raatibah na mwishoni nikakumbuka jambo ambalo linahitajia mimi kuswali swalah ya Istikhaarah – je, inafaa katika hali hiyo kuomba du´aa ya Istikhaarah au ni lazima kunuia jambo hilo kabla ya kuanza swalah yangu?

Jibu: Ni lazima kunuia jambo hilo kabla ya kuanza swalah yako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 186
  • Imechapishwa: 04/07/2022