44. Imamu anayetatizwa au kusoma makosa anatakiwa kusahihishwa

Imamu akitatizika na kusoma kimakosa, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesunisha kwa waswaliji kumrekebisha. Wakati mmoja pindi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaswali ambapo kisomo kikamtatiza. Alipomaliza akamwambia Ubayy:

“Je, wewe umeswali pamoja na sisi?” Akasema: “Ndio.” Ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Kwa nini hukunisahihisha?”[1]

[1] Abu Daawuud, Ibn Hibbaan, at-Twabaraaniy, Ibn ´Asaakir (2/296/2) na adh-Dhwiyaa’ katika ”al-Mukhtaarah” kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 111
  • Imechapishwa: 17/02/2017