45. Du´aa ya kumfukuza shaytwaan na wasiwasi wake

  Download

141-

1- “Kutaka kinga kwa Allaah dhidi yake.”[1]

2- “Kuadhini.”[2]

3- “Kufanya Adhkaar na kusoma Qur-aan.”[3]

[1] Abu Daawuud (01/620) na at-Tirmidhiy (01/282). na angalia: Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (01/77) na tazama pia Suurah “al-Mu´minuun” Aayah 98-99.

[2] Muslim (01/291) na al-Bukhaariy (01/151).

[3] ”Msiyafanye makaburi yenu kuwa ni makaburi.” Muslim (01/539).

Miongoni mwa mambo yanayomfukuza shaytwaan ni Adhkaar za asubuhi na jioni, za kulala na kuamka. Pia Adhkaar za kuingia na kutoka nyumbani, Adhkaar za kuingia na kutoka msikitini na Adhkaar nyenginezo zilizosuniwa kama mfano wa kusoma Aayat-ul-Kursiy wakati wa kulala, Aayah mbili za mwisho za al-Baqarah na pia yeyote mwenye kusema:

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْد، وهوَ على كلّ شَيءٍ قَدير

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake na himdi zote njema ni Zake na Yeye juu ya kila jambo ni muweza.”

mara mia moja, basi anakuwa na hifadhi kutokamana na shaytwaan siku yake nzima. Vilevile adhaana inamfukuza mbali shaytwaan.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 29/04/2020