Swali 40: Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya ijumaa ikikumbana na siku ya ´iyd? Je, itakuwa ni lazima kwa waislamu wote kuiswali au kikosi maalum? Wako watu wanaoamini kwamba ´iyd ikikutana na ijumaa basi hapo hakuna ijumaa[1].

Jibu: Ni lazima kwa imamu na khatwiyb waswalishe ijumaa na wahudhurie msikitini kuwaswalisha wale watakaohudhuria. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali ´iyd na ijumaa. Wakati mwingine akisoma katika ´iyd na ijumaa Suurah “al-A´laa” na “al-Ghaashiyah” katika swalah zote hizo mbili. Hayo yamesemwa na an-Nu´maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anh) kama ilivyothibiti katika “as-Swahiyh”.

Lakini yule mtu ambaye atahudhuria ´iyd inafaa kwake kuacha kuswali ijumaa na badala yake ataswali Dhuhr nyumbani kwake au pamoja na baadhi ya ndugu zake akiwa alihudhuria swalah ya ´iyd. Endapo ataswali ijumaa pamoja na wengine ndio bora na kamilifu zaidi. Na akiacha kuswali swalah ya ijumaa kwa sababu alihudhuria na kuswali ´iyd ni sawa kwake. Lakini ni lazima kwake kuiswali kwa aina ya Dhuhr. Ni mamoja atafanya hivo peke yake au na wengine.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/341-342).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 04/12/2021