Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ina nguzo moja, nayo ni “kumwabudu Allaah kama vile unamuona. Ikiwa wewe humuoni, basi Yeye Anakuona”. Dalili ya ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.” (an-Nahl 16:128)

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

”Tegemea kwa Mwenye nguvu kabisa, Mwenye kurehemu, ambaye anakuona wakati unaposimamama, na mageuko yako na wenye kusujudu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.” (ash-Shu´araa´ 26:217-220)

Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ

“Hushughuliki katika jambo lolote wala husomi humo chochote katika Qur-aan na wala hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo.” (Yuunus 10:61)

MAELEZO

Ihsaan ni kukamilisha ´ibaadah za nje na za ndani. Nako ni kule kumuabudu Allaah kama kwamba unamuona. Ikiwa wewe humuoni basi utambue kuwa Yeye anakuona. Atayetia hilo katika fikira yake wakati anapomuabudu Allaah basi ameihakikisha Ihsaan na amekusanya kheri zote. Allaah (Subhaanah) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.” (16:128)

إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ

“Hakika huruma wa Allaah uko karibu na wafanyao wema.” (07:56)

Kuna Aayah zengine zilizo na maana kama hii.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 44
  • Imechapishwa: 23/01/2017