36. Kumuosha maiti


28- Anapofariki maiti basi ni lazima kwa baadhi ya watu kuharakisha kumuosha. Kuhusu kuharakisha zimetangulia dalili zake katika kipengele cha tatu (masuala ya 17 nambari. 05) ukurasa wa 23-24.

Kuhusu ulazima wa kumuosha ni kutokana na amri yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth isiyopungua moja:

Ya kwanza: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Muhrim ambaye alivunjwa shingo yake na ngamia wake:

“Muosheni kwa maji yaliyochanganyikana na mkunazi… “

Tamko lake limekwishatangulia kwa ukamilifu wake na limetajwa katika masuala yaliyoashiriwa nambari. 04 ukurasa wa 22-23.

Ya pili: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu msichana wake Zaynab (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Muosheni mara tatu, au mara tano, au mara saba au zaidi ya hivo… “

Ukamilifu wake na takhriji yake yanakuja katika masuala yanayofuata.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 64
  • Imechapishwa: 17/02/2020