33. Watu bora ni wale ambao Mtume ametumilizwa kwao

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Watu bora baada ya watu hawa ni Maswahabah wengine wote wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); karne ambayo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumilizwa kwao. Wale waliotangamana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakamuona kwa macho (hata kama ni kwa muda mchache), wakamsikia na wakamuamini ni wabora kuliko wale waliokuja baadaye ambao hawakumuona hata kama watatenda matendo mazuri yote.”

MAELEZO

Dalili zenye kuonyesha kuwa Maswahabah ni bora kuliko wengine ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msiwatukane Maswahabah wangu. Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad imo mikononi Mwake lau mmoja wenu atajitolea dhahabu mfano wa mlima wa Uhud basi hatofikia vitanga viwili vya mikono vilivyojazwa na mmoja wao wala nusu yake.”[1]

Hii ni dalili inayofahamisha juu ya fadhilah yao kubwa mbele ya Allaah. Ole wa yule ambaye anawatukana au kuwakufurisha Maswahabah au kumponda mmoja katika wao. Tunaamini kwamba yule mwenye kufanya hivo ni mtu wa Bid´ah na mpotevu na mwenye kupotosha na atapata malipo yake mbele ya Mola wake.

Kuna makundi mawili ambayo yanawatukana Maswahabah:

1- Khawaarij. Wanawakafirisha Maswahabah wote isipokuwa tu Abu Bakr na ´Umar. Wanamkufurisha ´Aliy na wale idadi chache ya Maswahabah waliokuwa pamoja naye ambao wanasalimishwa mpaka na Raafidhwah.

2- Raafidhwah. Hawa wanawakufurisha Maswahabah wote isipokuwa tu ´Aliy bin Abiy Twaalib na idadi chache ya Maswahabah waliokuwa pamoja naye. Miongoni mwao ni Salmaan al-Faarisiy, ´Ammaar bin Yaasir na Abu Dharr. Si zaidi ya watu kumi. Wanawakufurisha wengine wote, bali akiwemo Abu Bakr na ´Umar mpaka yule Swahabah ambaye ni mdogo kabisa. Wanawakufurisha mpaka wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mama wa waumini, nao ni ´Aaishah bint Abiy Bakr na Hafswah bint ´Umar – Allaah awawie radhi wao na baba zao.

[1] al-Bukhaariy (3673) na Muslim (2541).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 135-136
  • Imechapishwa: 25/04/2019