32. Nifanye nini pindi nimepata ada ya mwezi katikati ya swalah?


Swali 32: Nifanye nini pindi nimepata ada ya mwezi katikati ya swalah?

Jibu: Ikitokea hedhi baada ya kuingia wakati wa swalah kwa mfano akapata hedhi nusu saa baada ya kupinduka kwa jua, basi atapotwahirika kutokamana na hedhi atatakiwa kulipa swalah hii ambayo wakati wake ulimkuta akiwa msafi. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]

Hatolipa swalah ndani ya kile kipindi cha hedhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth ndefu:

“Je, mwanamke anapopata hedhi si haswali wala hafungi?”

Wanachuoni wameafikiana kwamba hatolipa swalah zilizompita katika kipindi cha katikati ya hedhi. Ama atapotwahirika na kukawa kumebaki katika wakati kiwango kisichopungua kuiwahi Rak´ah moja, basi ataswali swalah ya wakati huo ambao ametwahirika ndani yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya swalah ya asubuhi kabla ya jua kuchomoza basi ameiwahi ´Aswr.”

Akisafika wakati wa alasiri au kabla ya kuchomoza kwa jua na akabaki juu ya hali hiyo mpaka jua kuzama au mpaka jua kuchomoza anaweza kuwahi kuswali Rak´ah moja, basi ataswali ´Aswr katika hali ya kwanza na Fajr katika hali ya pili.

[1] 04:103

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 29
  • Imechapishwa: 30/07/2021