30. Kuchinja karibu na maji ambayo watu wanaamini kuwa yanaponya

Swali: Kusini mwa Yordani kuna maji ya madini na ambayo yanaitwa ´kisima cha Sulaymaan bin Daawuud` ambayo watu huyakusudia kwa ajili ya kuyaoga na kutafuta ponyo na huja na vichinjwa kuvichinja wanapofika. Ni ipi hukumu ya kuchinja vichinjwa kama hivi?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa maji yamejaribiwa na kutambulika kuwa watu wananufaika nayo kutokana na baadhi ya magonjwa. Kwa sababu Allaah ameweka faida kwa baadhi ya maji kutokana na baadhi ya magonjwa. Likitambulika jambo hilo kwa majaribio ya kwamba maji hayo wananufaika nayo wale wenye maradhi fulani, kama romatizma na mengine, hakuna neno kufanya hivo.

Kuhusu vichinjwa ni jambo linahitaji upambanuzi. Ikiwa vinachinjwa kwa ajili haja zao kama vile kula na wageni wanaopata hapana vibaya. Ikiwa vinachinjwa kwa ajili ya sababu nyingine yoyote, kama kujikurubisha kwa maji haya, jini, Mtume au kwa kitu kingine katika imani mbovu ni jambo lisilojuzu. Kwa sababu Allaah (Subhaanah) amesema hali ya kuwa anamzungumzisha Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ

”Sema: “Hakika swalah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika; na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni muislamu wa kwanza.”[1]

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

“Hakika Sisi tumekupa al-Kawthar. Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako.”[2]

Kuchinja ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) pekee. Vivyo hivyo ´ibaadah nyenginezo zote ni kwa ajili ya Allaah pekee. Haijuzu kutekeleza chochote katika mambo hayo kumfanyia asiyekuwa Allaah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini kwa kujiengua na shirki na kuelemea Tawhiyd.”[3]

فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

“Mwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini. Zindukeni! Ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika.”[4]

Tukiongezea zile Aayah zilizotangulia na nyenginezo zenye maana kama hiyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amlaania mwenye kumchinjia asiyekuwa Allaah.”[5]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).

Haifai kwa mtu kumchinjia jini, nyota fulani, sayari fulani, maji fulani, Mtume fulani au mwengine yeyote au masanamu. Kujikurubisha anafanyiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa vichinjwa, swalah na ´ibaadah nyenginezo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

”Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.”[6]

Kutokana pia na yale yaliyotangulia katika maneno Yake (Jalla wa ´Alaa):

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.”[7]

فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

“Mwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini. Zindukeni! Ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika.”[8]

Na Aayah nyenginezo.

Kuchinja ni miongoni mwa ´ibaadah muhimu sana na ni miongoni mwa aina bora kabisa za kujikurubisha kwa Allaah. Kwa hivyo ni lazima kumtakasia Allaah pekee kutokana na zile Aayah tulizozitaja na yaliyotangulia katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah amlaania mwenye kumchinjia asiyekuwa Allaah.”[9]

[1] 06:162-163

[2] 108:01-02

[3] 98:05

[4] 39:02-03

[5] Muslim (1978).

[6] 01:05

[7] 98:05

[8] 39:02-03

[9] Muslim (1978).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 108-110
  • Imechapishwa: 13/07/2022