3- Mwendawazimu. Ni yule asiyekuwa na akili. Si lazima kwake kufunga kutokana na yale maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yaliyotangulia aliposema:

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu watatu; aliyelala hadi aamke, mdogo hadi awe mkubwa na mwendawazimu hadi apate fahamu.”

Swawm haisihi kwake kwa sababu hana akili ambayo ataweza kwayo kufahamu na kuinua ´ibaadah. Kwani ´ibaadah haisihi isipokuwa kwa nia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika matendo yote yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kwa lile alilonuia… “

Ikiwa wakati fulani anatokwa na akili na wakati mwingine zinamjia fahamu, basi atalazimika kufunga katika kile kipindi anapokuwa na ufahamu pasi na kile kipindi cha wendawazimu. Akitokwa na akili katikati ya mchana basi swawm yake haitoharibika. Ni kama ambavo atatokwa na ufahamu kwa sababu ya maradhi au kitu kingine. Kwa sababu alinuia funga akiwa na akili kwa nia sahihi. Isitoshe hakuna dalili ya uharibikaji na khaswa ikiwa inatambulika kuwa anapata fahamu anazipata saa maalum. Kujengea juu ya haya si lazima kwake kufungua siku ambayo aliondokwa na fahamu. Mwendawazimu akipata fahamu katikati ya mchana wa Ramadhaan basi atalazimika kujizuia siku iliobaki. Kwa sababu ameingia katika watu ambao wanawajibika kufunga. Si lazima kwake kufunga. Ni kama mfano wa mtoto anapobaleghe na kafiri anapoingia katika Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 44-4544-45
  • Imechapishwa: 22/04/2020