3. Mtoto asipewe jina lisilokuwa la kiarabu

Majina ya kigeni yenye kutoka katika miji ya kikafiri na ambayo yana maana yenye kukataliwa kidini na kilugha ni maasi kwa sababu jina liko hadharani na kwa kujiita nalo. Chini kuna mfano wa majina kama hayo:

1- Andre, Jacqueline, Julia, Diana, Suzana (lenye maana ya sindano au moto), Vally, Victoria, Coloria, Lara, Linda, Maya, Magnolia, Heidi na Yara.

2- Majina ya kigeni kama ya kiajemi, kituruki au ya kishenzi. Mfano wa hayo ni Mirfat, Jawdat, Haqqiy, Fawziy, Sherihan, Shirin, Nevin…

3- Majina yasokuwa na maana kama Zuzu, Vivvi, Mimmi…

4- Majina ya kimapenzi na laini kama Ahlaam, Ariyj, Taghriyd, Ghaadah, Faatin, Naahid, Huyaam (lenye maana ya hisia za upendo au ugonjwa wa ngamia) au Hayaam (mchanga huru).

Na kadhalika.

Ninahamiza kwa majina ya Shari´ah ya Kiislamu waislamu wote wamche Allaah, wajipambe kwa adabu ya Kiislamu na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wapuuzie majina hayo mabaya na wasiwaite watoto kwayo na hivyo wakaja kukosa mapambo yao, nayo ni majina ya Kishari´ah. Jambo hili lenye maradhi na lenye kuudhi ni wajibu kwa mtawala kulisitisha na ahakikishe kwenye mahakama hakuandikwi isipokuwa jina lililowekwa katika Shari´ah tu.

Ikiwa kwa mujibu wa sheria ya Ufaransa jina ni lazima liwe limedhibitiwa lisiende kinyume na historia na maadili yao na kama waislamu Bulgaria walilazimishwa kubadili majina yao ya Kiislamu, basi sisi tuna haki zaidi ya kushikamana bara bara na dini ya Allaah Uislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 04
  • Imechapishwa: 18/03/2017