27. Tofauti kati ya shirki kubwa na shirki ndogo

Kuna tofauti nyingi kati ya shirki kubwa na ndogo ikiwa ni pamoja na:

1- Shirki kubwa inamtoa mtu katika Uislamu. Upande mwingine shirki ndogo haimtoi mtu katika Uislamu. Lakini hata hivyo ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa. Isitoshe ni njia inayopelekea katika shirki kubwa.

2- Shirki kubwa inaharibu matendo yote. Kuhusu shirki ndogo inaharibu ktendo ambalo imechanganyika nayo na wala haiharibu matendo mengine ambayo hayakuchanganyika na shirki hii.

3- Shirki kubwa inahalalisha damu na mali tofauti na shirki ndogo. Shirki ndogo haihalalishi damu ya mtu na mali yake kwa sababu hajatoka katika Uislamu.

Wametofautiana wanachuoni kuhusu shirki ndogo, je, inasamehewa kama madhambi mengine ambayo ni chini ya shirki kubwa au haisamehewi kwa sababu Allaah amesema kwa jumla:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ

”Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa.”?

Hizi ndizo baadhi ya tofauti kati ya shirki kubwa na ndogo. Zote mbili ni khatari. Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Mtu asisemi kuwa ni shirki ndogo ambapo akachukulia sahali. Kwa ajili hii ndio maana ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:Hii inajumuisha shirki kubwa na ndogo. Lakini kuna tofauti kadhaa; shirki kubwa inamdumisha mwenye nayo Motoni milele na shirki ndogo haimdumishi mwenye nayo Motoni milele. Lakini hata hivyo ni lazima kwa mwenye nayo aadhibiwe na wala Allaah hakubali msamaha. Pamoja na hivyo hatodumishwa Motoni milele.

“Kuapa kwa Allaah hali ya kuwa ni mwenye kusema uongo kunapendeza zaidi kwangu kuliko kuapa kwa asiyekuwa Allaah hali ya kuwa ni mwenye kusema ukweli.”[1]

Kwa sababu dhambi ya kusema uongo ni ndogo kuliko dhambi ya shirki.

[1] Ameipokea ´Abdur-Razzaaq katika ”al-Muswannaf” (15929), at-Twabaraaniy (8902). al-Hawthamiy amesema:

“Wapokezi wake ni wapokezi Swahiyh.” Majmuu´-uz-Zawaa-id (04/177).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 49-51
  • Imechapishwa: 02/08/2018