Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa baadhi ya Maswahabah wana vyeo ambavyo wengine hawana. Ni wajibu kuwateremsha vyeo vyao. Akiwepo Swahabah ambaye anatoka katika familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kama ´Aliy bin Abiy Twaalib, Hamzah, al-´Abbaas, Ibn ´Abbaas na wengineo – basi hakika sisi tunawapenda zaidi kuliko wengine. Kwa sababu ya ule udugu wao na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hilo sio kwa njia ya kuachia. Tunatambua haki yake kwa kule kuwa na udugu na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hata hivyo haipelekei kwetu kumfadhilisha moja kwa moja juu ya wengine miongoni mwa wale ambao wana huduma kubwa katika Uislamu zaidi kuliko huyu ambaye ni ndugu yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu ngazi na fadhilah ni sifa ambazo mtu anaweza kusifika na moja wapo ambayo mwengine hana.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 21/08/2019