Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kutaka kinga ni Kauli Yake (Ta´ala):

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ

”Sema: “Najikinga na Mola wa mapambazuko.” (al-Falaq 113 : 01-02)

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

”Sema: “Najikinga na Mola wa watu.” (an-Naas 114 : 01)

MAELEZO

Kuomba kinga inahusu kumuomba Allaah kinga dhidi ya shari na kuelekea Kwake. Amesema (Ta´ala):

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ

“Sema: “Najikinga na Mola wa mapambazuko.”” (113:01)

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

“Sema: “Najikinga na Mola wa watu.”” (114:01)

Allaah anatakiwa kuombwa kinga dhidi ya shaytwaan na vyengine vyote vyenye kudhuru na adui. Ni jambo limeamrishwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

“Pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan, basi mtake kinga Allaah. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.” (07:200)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 36
  • Imechapishwa: 28/12/2016