25. Uokovu wakati wa kutokea tofauti

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nakuusieni kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mtumwa. Hakika yule atakayeishi zaidi katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti nyingi kabisa. Hivyo basi jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu. Ninakutahadharisheni na mambo ya kuzua, hakika kila kitachozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.” Ahmad (4/287), Abuu Daawuud (4753), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (42). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Mishkaah” (131).

Wakati wa tofauti watu wanatakiwa kurejea katika uongofu wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wa makhaliyfah. Amewaeleza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba makhaliyfah hawa ni waongofu na ni wenye kuongoza. Uongofu huu unatakiwa kufuatwa. Amesema kuwa (Radhiya Allaahu ´anhum) ni waongofu na akawatakasa kutokamana na upotevu bila ya ujuzi na upotevu kwa ujuzi. Allaah awawie radhi! Kwa hiyo wao ni wachaji, waongofu na watakasifu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaelekeza wale wakweli na wenye nia safi katika ´Aqiydah yake na ya watu hawa waongofu (Radhiya Allaahu ´anhum) pindi mapote yatapotofautiana.

´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) ana fadhila nyingi. Fadhila za Maswahabah kwa jumla zimeandikwa kwenye vitabu vingi. Hakuna kitu chochote kinachozungumzia ´Aqiydah isipokuwa ndani yake kimetaja fadhila za Maswahabah. Vilevile kuna vitabu vilivyoandika mambo hayo ikiwa ni pamoja vilevile na:

1- Fadhwaail-us-Swahaabah cha Imaam wa Ahl-us-Sunnah Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah).

2- Ma´rifat-us-Swahaabah cha Abu Nu´aym.

3- al-Iswaabah cha Ibn Hajar.

4- al-Istiy´ab cha Ibn ´Abdil-Barr.

5- Usd-ul-Ghaabah cha Ibn-ul-Athiyr.

Vitabu vyote hivi zinawazungumzia Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) ambavyo vimebainisha usuhuba na fadhila zao. Allaah awawie radhi wote!

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 15/10/2016