Ibn Abiy Haatim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Maswahabah wote wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kizazi chake wanatakiwa kutakiwa rehema na kunyamazia yale yaliyopitika kati yao.”

Inatakiwa kumuomba Allaah awawie radhi Maswahabah. Hilo ni tofauti na madhehebu ya Khawaarij, Raafdhwah na Nawaaswib.

Kuna Khawaarij wanaowakufurisha Maswahabah baada ya Abu Bakr na ´Umar kama mfano wa ´Uthmaan na ´Aliy.

Mu´tazilah wanawatukana wale walioshiriki katika vita kati ya ´Aliy na Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhum) na wanasema vibaya uaminifu wao.

Raafidhwah wanawatukana Maswahabah wote (Radhiya Allaahu ´anhum) isipokuwa wachache tu; ´Aliy, Bilaal, ´Ammaar, Salmaan na al-Miqdaad. Hivi ndivyo wanavyosema. Wanamkufurisha Abu Bakr na ´Umar na wanasema kwa kukata kabisa ya kwamba wataingia Motoni. Allaah awalipe kile wanachostahiki. Ni makafiri! Wanamkufurisha Abu Bakr na ´Umar na wanaonelea kuwa wao ndio watu wataopata adhabu kali Motoni kwenye tabaka ya chini kabisa. Ni madajali na ni waongo. Tunamuomba Allaah awaingize wao katika tabaka ya chini kabisa Motoni. Kwa sababu wao ni mazandiki na wanafiki. Wanafiki ndio wataoingia katika tabaka ya chini kabisa Motoni. Tunamuomba Allaah awafufue pamoja na wanafiki.

Hata Khawaarij wanawatukana Maswahabah, lakini sio kama Raafidhwah. Ukiongezea ya kwamba Raafidhwah wanawachukia Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), wamekusanya fikira za Jahmiyyah, Mu´tazilah na Khawaarij. Wao wana mabalaa yote.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 15/10/2016