22. Walinde watoto na wanafunzi wako


Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Tambua kwamba mioyo mema zaidi ni ile bora zaidi katika kupokea kheri. Mioyo ambayo kuna matarajio zaidi juu yake ni ile ambayo haijatanguliwa kufikiwa na shari.

MAELEZO

Mioyo migumu na ambayo haikubali mafunzo ni yenye kunyimwa. Amesema:

“Mioyo ambayo kuna matarajio zaidi juu yake ni ile ambayo haijatanguliwa kufikiwa na shari.”

Aidha moyo ambao haushawishiki na mambo yenye kuzuliwa ya leo na mambo yenye kupelekea katika shari, kukiwemo redio, runinga, intaneti na majanga mengine yalioko kati ya watu na yamekuwa mpaka mikononi mwa watoto. Yako mikononi mwa kila mmoja. Hizi ni njia za shari. Tayari zimekwishawafikia nyoyo za vijana na hivyo ni vigumu kuviondosha kutoka kwa vijana. Lakini endapo wangezuiwa navyo mara moja tokea mwanzo, mioyo yao ingelikuwa yenye kukubali haki na yenye kusalimika kutokamana na shari. Ni lazima kuzijaza nyoyo zao kheri na kuziepushia shari. Mshairi amesema:

Matamanio yake yamenifikia kabla sijajua ni kitu gani matamanio

yakaingia moyoni mwangu uliokuwa mtupu na yakakita

Ni lazima kuzinduka jambo hili. Ni janga kuona kwamba shari inazitangulia nyoyo kabla ya kheri. Kwa hiyo inakuwa vigumu kuiondosha kutoka moyoni. Kwa ajili hiyo wachunge watoto wako na wanafunzi wako na waepushe kutokamana na mambo ya shari. Ni mengi yaliyoje hii leo! Ni uchache ulioje mambo ya kheri! Vijana wa waislamu hii leo wako kwenye khatari kubwa kwa sababu mambo ya kheri ndio yaliyoenea na yamekuwa mikononi mwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 12/07/2021