22. Ni sawa kwa daktari anataka kwenda kuwashtaki wagonjwa walioathirika na madawa ya kulevya?

Swali 22: Wakati mwingine najiwa na baadhi ya wagonjwa ambao wamekunywa vilevi na madawa ya kulevya na matokeo yake wakaenda kufanya uhalifu kama wa uzinzi na liwati. Je, niwashtaki au hapana?

Jibu: Ni lazima kwako kuwanasihi. Wanasihi, wahimize kufanya tawbah na wasitiri na wala usende kuwashtaki na kuwafedhehesha. Vilevile wasaidie juu ya kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Waeleze kuwa Allaah (Subhanaah) anamsamehe mwenye kutubia na pia watahadharishe kurudi katika maasi haya. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao; wanaamrisha mema na wanakataza maovu… ”[1]

وَالْعَصْرِ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ

“Naapa kwa alasiri. Hakika mwanadamu bila shaka yumo katika khasara. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema na wakausiana haki na wakausiana subira.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dini ni kupeana nasaha.”

“Mwenye kumsitiri muislamu basi Allaah atamsitiri duniani na Aakhirah.”

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

[1] 09:71

[2] 103:01-03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 25/08/2019