Ni ipi hukumu ya kuwachukua picha viumbe waliokufa?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuwachukua picha wanyama waliokufa?

Jibu: Haijuzu ikiwa ni picha za viumbe walio na roho. Ni mamoja wameshakufa au wako hai. Haijuzu kuwachukua picha viumbe walio na roho. Tunaokusudia ni wale viumbe walio na roho kama mfano wa nyoka, nge, wadudu, ndege, wanadamu na wengineo. Hata hivyo hakuna neno kuwachukua picha viumbe wasiokuwa na roho. Tunaokusudia ni kama mfano wa miti, mito, bahari, majengo na magari. Hawa si kama wanadamu na hivyo hawana ubaya [kuwachukua picha].

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (12) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191546
  • Imechapishwa: 25/08/2019