Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya utegemeaji ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Na kwa Allaah Pekee tegemeeni ikiwa nyinyi ni Waumini!” (al-Maaidah 05 : 23)

وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

“Na yeyote yule atakayemtegemea Allaah, basi Yeye Humtosheleza.” (at-Twalaaq 65 : 03)

MAELEZO

Vilevile kutegemea ni ´ibaadah. Kutegemea maana yake ni kumuachia mambo Allaah na kumtegemea Allaah katika kila jambo pamoja na kufanya sababu. Unamtegemea Allaah ili kusalimika na shari, kuwa na amani na fitina, kupata riziki, kuingia Peponi na kuokoka kutokamana na Moto pamoja na kufanya sababu zilizowekwa katika Shari´ah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Na kwa Allaah pekee tegemeeni ikiwa nyinyi kweli ni waumini.” (05:23)

وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

“Na yeyote anayemtegemea Allaah, basi Yeye humtosheleza.” (65:03)

Ina maana kuwa Allaah humtosheleza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 35
  • Imechapishwa: 14/12/2016