21. Mitazamo mbalimbali ya watu juu ya karama


Watu wamegawanyika mafungu matatu katika maudhui ya mambo yasiyokuwa ya kawaida:

1 – Wako ambao wanapinga mambo hayo kutokea kwa wasiokuwa Mitume na pengine wakawa ni wenye kuyasadikisha kwa jumla na wakakadhibisha yale wanayotajiwa kuhusu watu wengi kwa sababu yeye anaona kuwa sio katika mawalii.

2 – Wengine wanaona kuwa kila ambaye anafanya jambo lisilokuwa la kawaida basi ni walii wa Allaah.

Yote mawili ni makosa… Kwa ajili hiyo utaona watu hawa wanataja namna ambavo washirikina na mayahudi na manaswara wana wasaidizi wanaowasaidia dhidi ya waislamu na kwamba eti ni katika mawalii wa Allaah. Upande wa pili wanakadhibisha kuweko na yeyote ambaye ana uwezo wa kufanya jambo lisilokuwa la kawaida.

Maoni ya sawa ni ya 3- wako pamoja nao wenye kuwanusuru katika jinsia yao na sio  katika mawalii wa Allaah.

Katika haya yaliyonukuliwa yanatosheleza – Allaah (Ta´ala) akitaka. Yule anayetaka zaidi basi arejee katika kile kitabu cha asli. Allaah ndiye Mwenye kuwafikisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 33
  • Imechapishwa: 28/06/2021