20. Watu wachukue msimamo gani kwa mtu ambaye ni khunthaa?

Swali 20: Khunthaa ataamiliwe matangamano ya mwanamke pamoja na kuzingatia kwamba jambo lake halijabainika? Je, yanamgusa yale yote yanayomgusa mwanamke kama mfano wa eda na mengineyo yanayowahusu wanawake?

Jibu: Kuna upambanuzi inapokuja kwa ambaye ni khunthaa. Khuthaa kabla ya kubaleghe anachanganya na hajulikani kama ni mvulana au msichana. Kwa sababu anakuwa na tupu mbili; tupu ya kike na tupu ya kiume. Lakini baada ya kubaleghe mara nyingi hubainika uume wake au uke wake. Kukibainika mambo yenye kuonyesha kuwa ni mwanamke – kwa mfano yakachomoza matiti yake au yakadhihiri kwake mambo yenye kumpambanua kutokamana na wanaume kwa mfano kutokwa na hedhi au mkojo kutoka kwenye njia na tupu ya kike – huyu anahukumiwa kuwa ni mwanamke. Tupu yake ya kiume itaondoshwa kwa njia za kimatibabu ambazo ni salama. Na kukidhihiri kwake yenye kufahamisha kuwa ni mvulana – kwa mfano ameota ndevu, kukojoa kutoka kwenye njia na tupu ya kiume na mengineyo ambayo yanajulikana na madaktari – basi ni mvulana na atataamiliwa matangamano ya wanaume. Kabla ya hapo watu wachukue msimamo wa kukomeka mpaka kwanza mambo yabainike. Asioe wala asiolewe mpaka kwanza mambo yabainike kama ni mvulana au msichana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 43
  • Imechapishwa: 17/08/2019