20. Dalili ya kumi na nane kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

18- Abul-Fath bin al-Battwiy ametuhathia: Abul-Fadhl bin Khayruun ametuhathia: Abu ´Aliy bin Shaadhaan ametuhathia: Abu Sahl bin Ziyaad ametuhathia: al-Qaadhwiy Ahmad bin Muhammad al-Bartwiy ametuhathia: al-Qa´nabiy ametuhathia: al-Mughiyrah bin ´Abdir-Rahmaan al-Qurashiy ametuhathia, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa al-A´raj, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swall Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati Allaah (´Azza wa Jall) alipohukumu viumbe aliandika katika kitabu Chake kilichoko Kwake juu ya ´Arshi: Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”[1]

Katika upokezi wa Abu Hurayrah imekuja ya kwamba alimsikia Mtume wa Allaah (Swall Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Allaah kabla hajaumba aliandika: “Hakika huruma Yangu inashinda ghadhabu Zangu.”Kiko Kwake juu ya ´Arshi.”

Imepokelewa na al-Bukhaariy na Muslim.

[1] al-Bukhaariy (3194), Muslim (2751), Ahmad (2/358), Ibn Maajah (4295), Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 57, al-Aajurriy katika ”ash-Shariy´ah”, uk. 290, Ibn Abiy ´Aaswim (608) na al-Answaariy katika ”al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd” (12).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 98
  • Imechapishwa: 02/06/2018