2- Maana yake: Kilugha maana yake ni usafi na kujisafisha na uchafu.

Maana yake kidini ni kuondosha hadathi na uchafu.

Makusudio ya kuondosha hadathi ni kuondosha sifa inayomzuia mtu kuswali kwa kutumia maji mwili mzima ikiwa hadathi hiyo ni kubwa. Ama ikiwa hadathi hiyo ni ndogo inatosha kutawadha. Maji yakikosekana au mtu akashindwa kuyatumia basi atatumia kile chenye kukaa mahala pake ambacho ni udongo kwa sifa iliyoamrishwa Kishari´ah. Jambo hilo litatajwa katika mlango wa Tayammum.

Makusudio ya kuondosha uchafu ina maana ya kuondosha najisi kutoka mwilini, nguo na maeneo.

Twahara ya kihisia imegawanyika aina mbili:

Ya kwanza: Twahara ya hadathi. Ni maalum juu ya mwili.

Ya pili: Twahara ya uchafu. Inakuwa juu ya mwili, nguo na maeneo.

Hadathi imegawanyika aina mbili:

Hadathi ndogo: Ni ile hali inayomuwajibishia mtu kutawadha.

Hadathi kubwa: Ni ile hali inayomuwajibishia mtu kuoga.

Uchafu umegawanyika aina tatu:

Ya kwanza: Kuna uchafu ambao ni lazima kuuosha.

Ya pili: Uchafu ambao ni lazima kuukwangura.

Ya tatu: Uchafu ambao ni lazima kuufutafuta.

[1] 09:28

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 1
  • Imechapishwa: 10/02/2020